Trakti
Je umewahi kwa wakati wo wote kumsikia mtu fulani akiita jina lako na hukujua mahali sauti hiyo ilikokuwa ikitoka? Au inawezekana hukuweza kuisikia sauti hiyo, kwa sababu kulikuweko na sauti nyingi kila upande. Sikiliza, sauti inakuita. Wewe! Wewe ni nani? Jina lako ni nani? Ulitoka wapi? Unaishi wapi? Unakwenda wapi? Unajua jina la kijiji chako. Inawezekana, hujawahi kwenda mahali pengine po pote. Lakini unafahamu kuwa kijiji chako ni sehemu ya nchi kubwa, na nchi zote ni sehemu ya ulimwengu mkubwa.
Tunaishi katika ulimwengu ambamo kila mmoja hupenda kutoa udhuru. Karibu kwa kila jambo linalogusa moyo wako hutaki kukubali au kuukabili ukweli jinsi ulivyo, kwa hiyo unatafuta njia ya kujitetea, ukidhania kwamba utetezi wako utakuweka huru. Je, unafikiri udhuru zako zitakuweka huru mbele za Mungu? Je, kuokolewa kunao udhuru? Visingizio ulivyo navyo kwa uhakika havitakuweka huru. Adamu na Hawa walipotenda dhambi, kila mmoja alijaribu kumwekea mwenzake lawama ya dhambi iliyotendeka, wakidhania kwamba Mungu angeachilia dhambi yao kwani wametoa sababu ni kwa nini waliingia dhambini. Lakini bado twasoma katika Biblia kwamba Mungu aliendelea kuwaadhibu tu. Mungu hazikubali udhuru zetu, hata zipangiwe kwa hila ya namna gani, au hata ukijifanya uonekane kuwa msafi kiasi gani. (Mwanzo 3:9-19; Wagalatia 6:7-8).
Bwana Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wanadamu kutoka kwa dhambi zao. “Bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa akawa ana mfano wa wanadamu” (Wafilipi 2:7). Alikufa kwa ajili ya dhambi za watu wote ulimwenguni, alizikwa na akafufuka tena (1Wakorintho 15:4), kisha akapaa kwenda mbinguni tena (Matendo 1:9). Mitume walimwona na pia waumini zaidi ya mia tano, baada ya kufufuka. Baada ya kupaa kwenda mbinguni, malaika wawili waliwaambia mitume kwamba kurudi kwake kutafanana na kupaa kwake. Ni Mungu tu ndiye anayefahamu ni lini Bwana atarudi. Huenda itakuwa ni jioni au usiku wa manane, au wakati wa asubuhi au alasiri. (Marko 13:35) “Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja” (Mathayo 24:44).