Je umewahi kwa wakati wo wote kumsikia mtu fulani akiita jina lako na hukujua mahali sauti hiyo ilikokuwa ikitoka? Au inawezekana hukuweza kuisikia sauti hiyo, kwa sababu kulikuweko na sauti nyingi kila upande. Sikiliza, sauti inakuita. Wewe! Wewe ni nani? Jina lako ni nani? Ulitoka wapi? Unaishi wapi? Unakwenda wapi? Unajua jina la kijiji chako. Inawezekana, hujawahi kwenda mahali pengine po pote. Lakini unafahamu kuwa kijiji chako ni sehemu ya nchi kubwa, na nchi zote ni sehemu ya ulimwengu mkubwa.
Biblia
Ilikuwa ni karibu miaka 6,000 iliyopita wakati ulimwengu ulipoumbwa. Uliumbwa na Mungu. Mungu ana Kitabu kiitwacho Biblia, ambacho kinaelezea jinsi alivyoumba ulimwengu na jinsi alivyomwumba mwanamume na mwanamke wa kwanza. Mungu alimwumba mwanadamu katika mfano Wake. Tangu wakati huo watoto wamezaliwa. Tangu wakati huo watu wamekufa. Maelfu kwa maelfu wamezaliwa na wamekufa. Ulizaliwa kutokana na baba na mama yako. Lakini kusema kweli ni Mungu aliyekuumba. Aliumba kila kitu. Je, umewahi kufikiria jinsi Mungu alivyoumba kila kitu kwa njia ya ajabu na jinsi alivyokuumba wewe? Wazazi wako walikupa jina. Mungu anajua jina lako. Anajua kila jina, hata liwe katikalugha gani. Anajua kila kitu. Kwa sababu Mungu alituumba anajua yote juu yetu. Anatupenda kwa sababu sisi ni Wake. Yeye ni Baba yetu aliyeko Mbinguni, na anatushughulikia zaidi kuliko baba na mama zetu wanavyofanya.
Mungu
Mungu amekuwepo wakati wote. Anaishi milele. Hivyo, wakati alipopulizia pumzi ndani yetu, pumzi hiyo ilitufanya pia tuishi milele. Hapana, sio miili yetu, kwa kuwa inakufa, bali roho ndani yetu inaishi milele. Je unamjua Mungu? Labda unauliza, "Mungu ni nani? Yuko wapi?" Je unataka kwa kweli kujua? Ndio, unataka. Ndani yako unataka kujua. Hujawahi kumwona Mungu, sivyo? Hapana, lakini hive haina maana kuwa Yeye hayuko. Kuna Mungu mmoja tu. Hakuna nafasi kwa ajili ya mwingine ye yote, kwa sababu Yeye ambaye ni Mungu kweli kweli anaenea Mbinguni na duniani. Yeye yupo mahali pote kwa wakati wote. Maskani ya Mungu ni Mbinguni, mahali pazuri hapo pa juu, lakini anaishi pia ndani ya mioyo ya watu ambao huitii sauti Yake. Nitajifunzaje kumjua Mungu? Je hilo ndilo swali unalojiuliza. Mungu anao mpango wa ajabu wa kutuonyesha jinsi. Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee, Yesu, duniani kutoka Mbinguni kuwaonyesha wana damu kuwa Yeye ni nani najinsi Alivyo. Mungu na Yesu ni Wamoja. Kwa muujiza, Mwana wa Mungu alizaliwa kama mtoto mchanga na alikua hadi kuwa mtu mzima. Kisha kwa miaka mitatu, Yesu au waambia watu kuhusu upendo wa Mungu, Baba Yake. Aliwaambia kuwa Mungu ni mtakatifu na hawezi kuvumilia kuona dhambi. Kisha Mungu alitayarisha njia kwa ajili yetu ili tupate kuokolewa kutoka katika dhambi zetu. Aliruhusu Mwana Wake Yesu kupigiliwa msumari msalabani na watu wenye dhambi. Aliutoa uhai Wake —upendo Wake mkubwa ulikuwa! Alikuwa ni sadaka ambayo inaweza kulipa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote-kila dhambi uliyoweza kutenda, kila dhambi ya kila mvulana, au msichana, mwanaume, au mwanamke. Je Yesu alibakia msalabani? Je Yesu alibakia kaburini? Hapana, baada ya siku tatu alifufuka kwa ushindi. Kisha alirudi tena Mbinguni na anangojea hadi Mungu anaposema ulimwengu ufikie mwisho. Kisha atakuwa Hakimu wa haki wa watu wote. Je unayo Injili ya Yohana? Soma sura ya 10. Yohana ameandika kite Yesu alichowaambia watu. Alichosema bado ni kwa ajili yetu leo. Yesu alisema Yeye alikuwa ni Mchungaji mwe ma na alitoa uhai Wake kwa ajili ya kondoo. Sisi ndio kondoo. Wale ambao ni kondoo Wake huijua sauti Yake! Naye huwaita kwa majina yao. Mgeni hawatamfuata.
Mgeni, Sauti He Nyingine
Ni nani huyo mgeni ambaye tutamkimbia? Ah, yeye ni mwizi! Hawajati kondoo. Yeye ni mwongo. Hakuna ukweli ndani yake. Yeye ni Shetani. Ni adui wetu, Shetani. Lakini kwanza, yeye ni adui wa Mungu. Wakati mmoja alikuwa ni malaika mwema pamoja na Mungu Mbinguni. Lakini alikuja kuwa na kiburi na kujikweza mwenyewe dhidi ya Mungu. Atipigana dhidi ya Mungu na malaika wengi watimwunga mkono. Mungu alishinda, kwa sababu ana uwezo wote. Hivyo, Anaweza kumtupa Shetani na wafuasi wake wote kutoka Mbinguni. Shetani anamchukia Mungu kwa ajili hii. Kwa sababu hawezi kamwe kumkaribia Mungu tena, anamwaga hasira yake juu ya viumbe vya Mungu, watu wa ulimwengu. Kwa sababu alitenda dhambi anajaribu kumshawishi kila mmoja atende dhambi. Kamwe dhambi haitaingia Mbinguni tena. Kuna mahali pengine, mahali ambapo Mungu alitengeneza kwa ajili ya Shetani na malaika zake. Nijehanamu. Jehanamu ni mahali pa mateso. Ni moto uwakao ambao kamwt hautazimika. Ni mahali ambako Shetani na wafuasi wake wataadhibiwa milele. Ni mahali pa kutisha ambako Mungu atapaswa atupeleke ikiwa tunachagua kuisikiliza sauti ya Shetani. Shetani hapendi sisi tufikirie juu ya jehanamu. Hapendi tufikirie juu ya Mungu. Hiyo ndio sababu anajaribu kuondosha uangalifu wetu kwa Mungu. Shetani anajaribu kutufanya tuisikilize sauti yake. Ndani kabisa yako, umeisikia He sauti nyingine, yingin sauti ya mgeni? Mara nyingine anatufanya tuamini ana mambo mema ya kutupa. Mara nyingine anatufanya tufikiri: "Mimi ni bora kuliko wengine. Mimi ni muhimu. Mimi kwanza. Nitasawazisha. Ni lazima kupigania haki zangu. Ni sawa kuiba, mradi sishikwi. Kila mmoja anasema uongo, hivyo na mimi naweza pia. Mawazo machafu sio mabaya sana - hakuna mtu anajua kile ninachowaza. Maneno machafu - ni mazuri kwa kicheko kikubwa." Na kwa nyakati nyingine je umekatishwa tamaa kiasi cha kujaribiwa kuwaza, "Mimi sifai, kwa nini niendelee kuishi?" Hizi zote ni sauti za Shetani. Yeye ni mwongo. Hiyo ndio sababu anajaribu kutufanya waongo pia. Yeye ni mwizi, hiyo ndio sababu anataka kutufanya tuibe pia. Yeye ni muuaji, hiyo ndio sababu anajaribu kutufanya tuwachukie wengine pia. Unapoisikiliza sauti hiyo, je inakufanya ujisikie vipi? Je inakufanya ujisikie vizuri ndani? Ah, hapana, inakufanya usiwe na raha. Inakufanya utake kujificha. Hivyo, ndivyo na Shetani alivyo. Anapenda kufanya mambo gizani.
Yesu, Sauti ya Mchungaji
Je, unamjua Yesu, Mchungaji Mwema? Ungependa kuwa kondoo wake? Ungependa kuijua sauti yake? Ah, ndio unaweza; Lakini, kwanza, ni lazima usisikilize tena sauti He nyingine. Sasa, wakati umetulia, utaisikia sauti ya upole ya Yesu ikikuita kumtolea maisha yako yote. Utamsikia akikuambia uzihuzunikie dhambi zako zote na kuzitubia. Labda, wakati fulani ulipokuwa umetulia kabisa, ulikuwa ukiwaza, "Nitafanya nini na matatizo yangu yote na mizigo? Natamani ningekuwa mwema. Natamani ningekuwa mahali ambapo kamwe singekuwa na njaa au mgonjwa tena. Je, kitatokea nini wakati nikifa? Na labda umewahi kuwa na mawazo mengi zaidi. Hiyo ni sauti ya Yesu ikikuita. Je mara nyingine unajisikia una huzuni hata wakati hujui sababu yake ni nini? Au unajisikia mpweke hata wakati huko peke yako? Mawezekana ni kwa sababu uko mpweke kwa ajili ya Mungu, Yeye ambaye alikuumba na anakupenda. Yeye ni Mchungaji anayeita kondoo aliyepotea. Anaita na anaita, na anatafuta na kukutafuta! Wakati unapoisikia sauti ya Mchungaji, mjibu. Mwambie unahuzunika kwa ajili ya dhambi zako. Mwambie jinsi unavyojisikia, na umwambie akuokoe. Hivyo ili kuomba. Je umewahi kuomba kwa Mungu wa Mbinguni? Fanya hivyo sasa. Atakusikia na kukuelewa. Atakupa amani ambayo unaitamani. Je hupendi kuwa kondoo Wake na kuijua sauti Yake? Anataka awe Rafiki yako. Atakuondolea mzigo wa dhambi. Utajisikia una furaha ndani. Utakuwa na upendo na mwema kama Yeye alivyo. Atakusaidia ushinde woga wako. Hata ikiwa wengine watalwfanyia dhihaka kwa kuwa Mkristo, unafahamu kuwa Yesu atakulinda. Hata ikiwa mgeni atakujaribu tena, ni lazima umtegemee Yesu kukusaidia kushinda. Wakati uko salama katika mikono ya upendo ya Mchungaji, unafahamu kuwa mwishoni atakufikisha kwenye Makao Yake ya ajabu, ya furaha pamoja na Mungu, kuishi pamoja Naye milele!